Skip to content
Ishara ya Ibrahim – Qur’an Ishara ya Ibrahim – Taurati (Mwanzo 12:1-7)
Surat 3:84 (Al Imram)Sema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na tuliyo teremshiwa sisi, na aliyo teremshiwa Ibrahim, na Ismail, na Is-haak na Yaakub na wajukuu zao, na aliyo pewa Musa na Isa na Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi. Hatubagui baina yao hata mmoja, na sisi ni wenye kusilimu kwake.

Surat 4:54 (The Women)

Au wanawahusudu watu kwa yale aliyo wapa Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake? Basi tuliwapa ukoo wa Ibrahim Kitabu na hikima na tukawapa utawala mkubwa.

Wito Wa Abramu

1BWANA akawa amemwambia Abramu, “Ondoka katika nchi yako, waache watu wako na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha. 2“Mimi nitakufanya taifa kubwa
na nitakubariki,
Nitalikuza jina lako,
nawe utakuwa baraka.
3Nitawabariki wale wanaokubariki,
na ye yote akulaaniye nitamlaani;
na kupitia kwako mataifa yote duniani
yatabarikiwa.”

4Hivyo Abramu akaondoka kama BWANA alivyokuwa amemwambia; naye Loti akaondoka pamoja naye. Wakati Abramu alipoitwa aondoke Harani, alikuwa na miaka sabini na mitano. 5Abramu akamchukua Sarai mkewe pamoja na Loti mwana wa ndugu yake, mali zote walizokuwa nazo pamoja na watu aliokuwa amewapata huko Harani, wakasafiri mpaka nchi ya Kanaani, wakafika huko.
6Abramu akasafiri katika nchi hiyo akafika huko Shekemu, mahali penye mti wa mwaloni ulioko More. Wakati huo Wakanaani walikuwa wanaishi katika nchi hiyo. 7BWANA akamtokea Abramu akamwambia, “Nitawapa uzao wako nchi hii.” Hivyo hapa Abramu akamjengea BWANA aliyekuwa amemtokea madhabahu.