Skip to content
Ishara ya Ibrahim (Sehemu ya 2) – Qur’an Ishara ya Ibrahim (Sehemu ya 2) – Taurati

Surat 37: 83-84,99-101 (The Saffat)

83. Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake,

84.Alipo mjia Mola wake Mlezi kwa moyo mzima.

99. Na akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Mola wangu Mlezi; Yeye ataniongoa.

100. Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema.

101.Basi tukambashiria mwana aliye mpole.

Mwanzo 15:1-6

Agano La Mungu Na Abramu

1Baada ya jambo hili, neno la BWANA likamjia Abramu katika maono:“Usiogope, Abramu.
Mimi ni ngao yako,
na thawabu yako kubwa sana.”

2Lakini Abramu akasema, “Ee BWANA Mwenyezi, utanipa nini na mimi sina hata mtoto na atakayerithi nyumba yangu ni huyu Eliezeri Mdameski?” 3Abramu akasema, “Hukunipa watoto, hivyo mtumishi katika nyumba yangu ndiye atakuwa mrithi wangu.”
4Ndipo neno la BWANA lilipomjia: “Mtu huyu hatakuwa mrithi wako, bali mwana atakayetoka katika viuno vyako mwenyewe ndiye atakayekuwa mrithi wako.” 5Akamtoa nje na kusema, “Tazama juu kuelekea mbinguni na uhesabu nyota, kama hakika utaweza kuzihesabu.” Ndipo akamwambia, “Hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.”
6Abramu akamwamini BWANA, naye kwake hili likahesabiwa kuwa haki.